Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kinapenda kuwataarifu waombaji kazi mbalimbali waliofanya usaili tarehe 2 hadi 4 Mei, 2026 kuwa, majina ya waombaji kazi waliofaulu usaili huo ni kama yalivyoorodheshwa katika tangazo hili.
Waombaji waliofaulu usaili watatakiwa kukamilisha taratibu mbalimbali za ajira kwa kufika, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) jengo la Utawala, Ofisi ya Masjala, Chumba Na. 315 siku ya Jumanne, tarehe 1 Septemba, 2026 kuanzia saa tatu kamili asubuhi, wakiwa na nyaraka zilizoainishwa katika tangazo hili ili ziweze kuhakikiwa kabla ya
kupewa barua za ajira.
Kwa wale ambao majina yao hayapo katika tangazo hili, watambue kuwa hawakupata nafasi/hawakufaulu usaili, hivyo wasisite kuomba kwa mara nyingine pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa.
Nyaraka za kuwasilisha ni kama ifuatavyo:
Vyeti halisi (Original Certificates and Transcripts) na nakala mbili za vyeti hivyo ambazo zimethibitishwa na Mamlaka za kisheria (certified by Advocate/Magistrate) vya masomo kuanzia kidato cha nne na kuendelea;
Cheti cha kuzaliwa; Nakala ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA); na Picha ndogo nne za rangi (four coloured passport size photographs)
DOWNLOAD PDF HAPA








Leave a Reply