MAJINA ya Walioitwa Kwenye Usaili Wakala wa Vipimo 27/07/2026

MAJINA ya Walioitwa Kwenye Usaili Wakala wa Vipimo 27/07/2026

Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA) anapenda kuwataarifu waombaji wa
nafasi za kujitolea zilizotangazwa tarehe 06 Juni, 2026 kuwa, usaili utafanyika tarehe 07,
Agosti, 2026 saa 1:30 asubuhi katika Ofisi za Wakala wa Vipimo Makao Makuu
Dodoma.
Wasailiwa wanaoitwa wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-
1. Usaili utafanyika kuanzia tarehe kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili muda na
sehemu ambapo usaili utafanyika umeainishwa.
2. Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;
3. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha
Mpiga kura, Kitambulisho cha kazi, Kitambulisho cha Uraia, Hati ya kusafiria, Leseni
ya Udereva au barua ya utambulisho kutoka Serikali ya Mtaa/Kijiji/shehia anakotoka
msailiwa.
4. Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa,
kidato cha IV, VI, Cheti cha Taaluma.
5. Wasailiwa watakaowasilisha Testimonials, Provisional Results, Statement of
results, hati za matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips)
HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI.
6. Kila msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi.
7. Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na
kuidhinishwa na Mamlaka husika (kama TCU, NACTVET au NECTA)
8. Waombaji ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa
hawakukidhi vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi zitakapotangazwa na
kuzingatia mahitaji ya tangazo husika.
9. MUHIMU: Wasailiwa watakao shindwa kuwasilisha nyaraka zilizokamilika kama
zilivyoainishwa katika kipengele na. 2, 3, 4 na 8 hawataruhusiwa kuendelea na usaili.

DOWNLOAD PDF YA MAJINA HAPA